YANGA-SIMBA-CAF

Simba, Yanga zasaka ushindi wa ugenini michuano ya CAF

-
- CAF

Timu za Simba na Yanga zimesafiri kwenda ugenini kwa ajili ya michezo ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho dhidi ya wapinzani wao.

Matangazo ya kibiashara

Yanga iliondoka nchini jana kuelekea Zimbabwe ambako keshokutwa itachuana na wapinzani wao Township Rollers katika mchezo wa marudiano wa ligi ya mabingwa Ulaya, huku ikiwa nyuma kwa mabao 2-1 iliyofungwa katika mchezo wa kwanza uliofanyika Jijini Dar es Salaam.

Yanga inahitaji ushindi wa mabao 2-0 ili kufuzu hatua inayofuata na itategemea zaidi washambuliaji wake Pius Buswita na Obrey Chirwa ambaye alifunga bao la kufutia macho zi kwenye mchezo wa kwanza.

Mshindi baina ya Rollers na Yanga atafuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya klabu barani Afrika.

Simba ambao ni wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho wameondoka nchini alfajiri ya leo kuelekea nchini Misri kwa mchezo wa marudiano dhidi ya wapinzani wao Al-Masry.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, timu hizo zilifungana mabao 2-2 huku Simba ikikomboa bao dakika za mwisho. Simba itategemea zaidi washambuliaji Emanuel Okwi na John Bocco.

Ili kufuzu hatua inayofuata Simba inahitaji kushinda mchezo huo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Port Said au kutoka sare ya kuanzia mabao 3-3.