Pata taarifa kuu
TANZANIA-DRC-FIFA

Tanzania, DRC zatambiana kuelekea mchezo wa kimataifa wa kirafiki

Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars wakiwa mazoezini
Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars wakiwa mazoezini
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Makocha wa Timu za Taifa za Tanzania 'Taifa Stars' Hemed Morocco na mwenzake wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo 'Leopards' Florent Ibenge wamesema timu zao ziko tayari kwa mchezo wa kimataifa wa kirafiki utakaochezwa kesho Jumanne katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Matangazo ya kibiashara

Mchezo huo ni sehemu ya michezo ya kimataifa ya kirafiki inayotambuliwa kwa mujibu wa kalenda ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Mjini Dar es Salaam, Kocha Mkuu wa Leopards, Florent Ibenge amesema anaamini Tanzania ni nzuri na ndio maana alichukua uamuzi wa kucheza nayo katika mechi ya kirafiki.

“Ni timu nzuri na tunatarajia mchezo mgumu na wenye upinzani,'amesema Ibenge na kuwataja wachezaji Mbwana Samatta, Simon Msuva na Thomas Ulimwengu kuwa ni wachezaji wazuri anaowafahamu. Hata hivyo Thomas Ulimwengu hatakuwemo kwenye kikosi cha Stars kwa sababu ya majeraha.

Kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Hemed Morocco kikosi chake kitamkosa kipa Aishi Manula na kiungo Abdul Makame.

“Wachezaji wote wako vizuri isipokuwa Manula na Makame, tutapigania ushindi kwenye uwanja wetu wa nyumbani,”amesema Morocco.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Clifford Mario Ndimbo, mchezo huop utaanza saa 10 alasiri na kiingilio cha chini ni shilingi shilingi 1000.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.