TANZANIA-DRC-FIFA

Ibenge aipongeza Taifa Stars kwa kuifunga DRC

Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo 'Leopards' Florent Ibenge ameipongeza tanzania kwa kuivuka na ushindi katika mchezo wa kirafiki dhidi ya DRC.

Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya DRC, Florent Ibenge.
Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya DRC, Florent Ibenge. ISSOUF SANOGO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Tanzania ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya DRC katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa jana katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam. Mabao ya Tanzania yalifungwa Mbwana Samatta na Shiza Kichuya.

Ibenge amesema Traifa Stars ilitumia majkosa madogo madogo ya timu yake na kufanikiwa kupata matokeo katika mchezo huo.

“Mechi ilikuwa nzuri na ngumu, Tannzania ilitusumbua kipindi cha pili hasa safu yao ya ushambuliaji,”amesema Ibenge.

Katika mchezo huo kocha Mkuu wa Taifa Stars Salum Mayanga, aliwatumia washambuliaji Simon Msuva anayechezea Difaa ElJadida ya Morocco, Shiza Kichuya wa Simba na nahodha Mbwana Samatta anayechezea KRC Genk ya Ubelgiji.

Kwa upande wake Samatta alisema Tanzania inaweza kushindana kisoka na mataifa makubwa ya Afrika ikiwa itakuwa na wachezaji wengi wanaocheza soka la kulipwa nje ya Tanzania.

“Kucheza nje kuna manufaa sana, wenzetu kikosi chao karibu chote kinacheza nje, ninaamini tukiwa na wachezaji wengi wa nje tutapata uzoefu zaidi na timu itaweza kushindana,”

Ushindi wa Taifa Stars unaweza kuipandisha kwenye viwango vya ubora duniani.