Pata taarifa kuu
MPIRA WA KIKAPU

Tanzania kuandaa michuano ya mpira wa kikapu ya Kanda ya tano Afrika

Basketball-Africa
Basketball-Africa REUTERS
Ujumbe kutoka: Emmanuel Richard Makundi | RFI
Dakika 2

Nchi ya Tanzania itakuwa mwenyeji wa michuano ya mpira wa kikapu ya kanda ya tano ya Afrika kwa wachezaji walio na umri chini ya miaka 18 itakayofanyika mwezi wa sita.

Matangazo ya kibiashara

Kanda ya tano Afrika hujumuisha nchi 12 ambazo ni Misri, Sudan, Sudan Kusini, Eritrea, Djibout, Kenya, Ethiopia, Uganda, Rwanda, Burundi na Tanzania wakaokuwa wenyeji.

Akizungumza na RFI Kiswahili katika mahojiano maalumu, rais wa Chama cha mpira wa kikapu Tanzania, TBF, Fares Magesa amesema hiyo ni fursa kwa Tanzania kujitangaza kupitia mchezo wa kikapu.

“Miaka ya nyuma tulishiriki mashindano mengi nje ya nchi lakini kwa sasa tumewasiliana na Shirikisho la mpira wa kikapu Afrika (Fiba) na wametuthibitishia kuwa tutaandaa. Ni fursa muhimu kwa Tanzania kukuza mpira wa kikapu,”alieleza.

Michuano hiyo itakayochezwa jijini Dar es Salaam itashirikisha timu 24m 12 za wanawake na 12 za wanaume.

Magesa pia amesema shirikisho lake litahakikisha linasimamia ligi za mikoa kwa kushiriki na viongozi wa mikoa ili kupata wachezaji wazuri watakaiwakilisha Tanzania katika michuano hiyo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.