KENYA-AUSTRALIA-MICHEZO

Kenya yaangushwa na Jamaica katika mbio za mita 3000

Kenya imekosa medali ya dhababu katika mbio za Mita 3000 kuruka viunzi na maji kwa upande wa wanawake, katika michezo ya Jumuiya ya Madola inayoendelea nchini Australia, baada ya Mjamaica Aisha Praught kumaliza wa kwanza kwa muda wa dakika 9 na sekunde 21.

mMashindano ya Commonwealth Games yanaendelea huko Australia.
mMashindano ya Commonwealth Games yanaendelea huko Australia. Anthony WALLACE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, Celliphine Chepteek Chespol alimaliza wa pili kwa muda wa dakika 9 na sekunde 22, huku Mkenya mwingine Purity Cherotich IRUI akimaliza kwenye nafasi ya tatu.

Matumaini ya kunyakua medali ya dhahabu sasa, yamehamia kesho wakati wa mbio za Mita 800 kwa upande wa wanaume.

Kenya itawakilishwa na Jonathan Kitilit na Wyclife Kinyamal.

Hadi sasa taifa hilo lina medali tatu za fedha na shaba, huku majirani Uganda wakifanya vema hadi sasa kwa kupata medali mbili za dhahabu baada ya Joshua Kiprui Cheptegei hivi karibuni kushinda mbio za Mita 5000 lakini pia Stella Chesang ambaye siku ya Jumatatu, alishinda mbio za Mita 10,000 kwa upande wa wanawake.