Pata taarifa kuu
ULAYA-SOKA

Klabu nne kuwania taji la klabu bingwa barani Ulaya

Kikosi cha klabu ya Bayern Munich.
Kikosi cha klabu ya Bayern Munich. REUTERS
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Liverpool, Bayern Munich, Roma na Real Madrid zimefuzu katika hatua ya nusu fainali kuwania taji la klabu bingwa barani Ulaya.

Matangazo ya kibiashara

Licha ya kutofungana, Bayern Munich ilifanikiwa kufika katika hatua hiyo jana usiku kwa jumla dhidi ya Sevilla ya Uhispania.

Nayo Real Madrid ilipata ushindi mwembamba wa jumla ya mabap 4-3 dhidi ya Juventus ya Italiana kusonge mbele.

Leo usiku kuna michuano ya robo fainali ya kuwania taji la Europa League.

Ni michuano ya mzunguko wa pili ili kutafuta timu nne zitakazofuzu katika hatua ya nusu fainali.

CSKA Moscow itakuwa nyumbani dhidi ya Arsenal kujaribu kufuta kichapo cha mabao 4-1 walichopata ugenini.

Atletico Madrid nayo inakutana na Sporting CP baada ya kuishinda mabao 2-0 nyumbani huku Marseiile wakiwa nyubani kutafuta ushindi muhimu dhidi ya RB Leipzig ya Ujerumani iliyoifunga bao 1-0.

Lazio ambayo ilishinda Red Bull Salzburg ya Austria mabao 4-2 itakuwa inajitahidi kunedeleza ushindi au sare ili kusonga mbele.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.