TANZANIA-MAFURIKO-KASSIM MAJALIWA

Serikali ya Tanzania yasisitiza wananchi wake kuhama maeneo ya mabondeni

Serikali ya Tanzania imewendelea kusisitiza kuwa wananchi wanaoishi mabondeni kuhama katika maeneo hayo kutokana na mvua za masika zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini humo.

Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli. 12 Juni, 2017
Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli. 12 Juni, 2017 Ikulu/Tanzania
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo, bungeni Mjini Dodoma, Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ni vyema wananachi wakahama katika maeneo hayo na kwamba serikali ya nchi hiyo inaandaa fedha ili kuboresha miundombinu katika maeneo ya mabondeni.

"Mara kadhaa tumeshuhudia mvua hizi zinaponyesha zinaleta madhara kwa wananchi wanaokaa mabondeni,"amesema Majaliwa ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Ruangwa, Mkoani Lindi.

Aidha kiongozi huyo amewataka viongozi mbalimbali wa kisiasa kushirikiana na serikali katika kuhakikisha wananchi walioko maeneo ya mabondeni wanaondoka katika maeneo hayo.

RFI Kiswahili imezungumza na wananchi wanaoishi katika maeneo ya mabondeni, Mto Kizinga na Jangwani ambao wamesema licha ya kuathirika na mvua mara kwa mara lakini changamoto ya umaskini imekuwa kikwazo kwao kupata maeneo salam.

Hata hivyo idara ya hali ya hewa nchini humo, TMA imeonya licha ya kupungua kwa mvua bado maeneo ya ukanda wa pwani na mikoa ya kaskazini na kusini magharibi mwa nchini yataendelea kupata mvua.

Mvua zinazonyesha nchini Tanzania zimesababisha athari uharibifu wa mali na miundombinu huku mamlaka katika Jiji kuu la kibiashara la Dar es salaam, zikithibitisha watu 10 kupoteza maisha.