ARSENAL-SOKA-VIEIRA

Patrick Vieira: Niko tayari kuifunza Arsenal

Nahodha wa zamani wa klabu ya Arsenal Patrick Vieira amesema yuko tayari kuifunza klabu hiyo, iwapo atapewa nafasi hiyo.

Mchezaji wa zamani wa Arsenal Patrick Vieira
Mchezaji wa zamani wa Arsenal Patrick Vieira wikipedia
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, Vieira ameeleza klabu anayofunza kama kocha ya New York City FC, haijapata mawasiliano yoyote kutoka kwa uongozi wa Arsenal.

Raia huyo wa Ufaransa aliyezaliwa jijini Dakar Senegal, alianza kuifunza New York City FC kuanzia mwaka 2016, baada ya kutia saini mkataba wa miaka mitatu.

Aliwahi kuichezea Arsenal kati ya mwaka 1996-2005 na kuifungia mabao 29 katika mechi 279.

Vierra mwenye umri wa miaka 41, amewahi pia kuifunza Manchester City Reseverves

Arsenal inamtafuta kocha mpya , baada ya kocha wa muda mrefu Arsene Wenger kutangaza kuwa ataondoka katika klabu hiyo mwisho wa msimu wa ligi kuu nchini Uingereza. Amekua akfunza klabu hiyo kwa muda wa saa 22.

Wenger amewahi kunukuliwa akisema Vieira ipo siku atakuwa kocha wa Arsenal.

Makocha wengine ambao wametajwa kuwa katika nafasi ya kumrithi Wenger ni pamoja na Massimiliano Allegri, Carlo Ancelotti, Mikel Arteta,Luis Enrique, Leonardo Jardim, Joachim Löw, Brendan Rodgers, Diego Simeone

Miongoni mwa wengine wengi.