ARSENAL-WENGER-SOKA-MICHEZO

Arsene Wenger abadili kauli baada ya kutangaza kuondoka Arsenal mwisho wa msimu

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amebadili kauli yake siku moja baada ya kukubali kuondoka katika klabu hiyo mwisho wa msimu huu.

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger.
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger. Reuters/Scott Heppell
Matangazo ya kibiashara

Lakini amesema kuwa tangazo lililofanywa kuhusu kuondoka kwake katika klabu ya Arsenal siku ya Jumatano baada ya takriban miaka 22 haukuwa uamuzi wake.

“Haukua uamuzi wangu kuondoka Arsenal, “ amesema Wenger.

Wenger aliongezea kwamba atafanya kazi kama kawaida na kwamba hatochukua jukumu lengine kwa sasa.

Alikuwa akijibu swali moja kutoka kwa mwandishi wa Ujerumani aliyetaka kujua kwa nini alikuwa anajiondoa wakati huu kabla ya mechi kubwa.

Awali katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Wenger amesema:

"Baada ya kutafakari na kufanya mazungumzo na klabu , nahisi ni wakati muafaka kujiuzulu mwisho wa msimu huu".

Baada ya Arsenal kupokea kichapo kwenye uwanja wa nyumbani wa Emirates, katika michuano ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Olympiakos, mashabiki wa klabu hiyo wamemtaka kocha wao, Arsene Wenger kuachia ngazi.

Katika mchezo huo ambao ulipigwa mwanzoni mwa wiki hii, Arsenal ilikubali kichapo cha mabao 3-2 na kuifanya klabu hiyo kushika nafasi ya mwisho katika kundi F ikiwa haina hata pointi na wakitarajia kukutana na Bayern Munich katika mchezo wao wa tatu.