Pata taarifa kuu
MAN UNITED-SOKA

Ferguson aendelea vema baada ya upasuaji wa ubongo

Alex Ferguson (kulia) na wachezaji wake wa Manchester United washerehekea ushindi wao Mei 13, 2013.
Alex Ferguson (kulia) na wachezaji wake wa Manchester United washerehekea ushindi wao Mei 13, 2013. AFP/ANDREW YATES
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 3

Ripoti kutoka Uingereza zinasema kuwa, kocha wa zamani wa Manchester United Alex Ferguson ameanza kuketi na amekuwa akizungumza na familia yake baada ya kufanyiwa upasuaji wa ubongo mwishoni mwa wiki iliyopita.

Matangazo ya kibiashara

Kocha huyo mwenye mafanikio zaidi katika soka ya Uingereza amebaki kitengo cha wagonjwa walio chini ya uangalizi maalum, lakini tangu Jumatatu wiki hii alikuwa anaweza kuketi na kuzungumza na wanafamilia yake na marafiki katika hospitali ya Salford Royal alikolazwa tangu Jumamosi.

Hakujawa na taarifa rasmi kuhusu hali ya kiafya ya kocha huyo mkongwe mwenye umri wa miaka 76, aliyestaafu mwaka 2013.

Wachezaji mbalimbali na makocha wa soka wamekuwa wakisema wana imani kuwa, Ferguson atapata nafuu hivi karibuni na kurejelea hali yake ya kawaida.

Ifahamu Manchester United chini ya usimamizi wa Fergusson

Manchester United ni klabu ya kandanda ya Uingereza, ambayo ni mojawapo ya vlabu maarufu sana ulimwenguni, na ina makao katika Old Trafford eneo la Greater Manchester. Klabu hii ilikuwa mwanachama mwanzilishi wa Ligi ya Primia mwaka 1992, na imeshiriki katika daraja ya juu ya kandanda ya Uingereza tangu mwaka wa 1938, isipokuwa msimu wa 1974-75. Mahudhurio ya wastani kwenye klabu yamekuwa ya juu kuliko timu nyingine yoyote katika kandanda ya Uingereza kwa misimu yote isipokuwa sita tangu 1964-65.

Manchester United ni miongoni mwa vlabu vyenye ufanisi mkubwa katika historia ya kandanda ya Uingereza na kimeshinda mataji makubwa 22 tangu Alex Ferguson alipochukua wadhifa wa meneja wake mnamo Novemba 1986. Mwaka wa 1968, ilikuwa klabu ya kwanza kushinda Kombe la Uropa kwa kucharaza Benfica 4-1. Walishinda kombe la pili la Ulaya kama sehemu ya ushindi wa mataji matatu mwaka 1999, na la tatu mwaka wa 2008, kabla ya kumaliza katika nafasi ya pili mwaka wa 2009. Klabu hihyo inashikilia rekodi mbili ya kushinda mataji mengi ya Ligi ya Uingereza mara 18 na pia kushikilia rekodi kwa wingi wa kutwaa kombe la FA ikiwa imeshinda mara 11.

Tangu mwisho wa mwaka ya 1990, klabu hiyo imekuwa mojawapo ya vlabu tajiri duniani ilio na mapato ya juu kuliko kiabu yoyote, na sasa inatajwa kama klabu yenye thamani zaidi katika mchezo wowote, na makisio ya thamani ya takriban bilioni £ 1.136 (sawa na Euro bilioni 1.319 ) Aprili 2009.Manchester United ilikuwa mwanachama mwanzilishi wa kundi la vlabu la G-14 la Vlabu kuu vya kandanda Uingereza, ambalo halipo tena, na European Club Association, muungano uliochukua nafasi yake.

Alex Ferguson amekuwa meneja wa kilabu hiyo tangu Novemba 6,1986 alipojiunga na Manchester United kutoka Aberdeen baada ya kung'atuka kwa Ron Atkinson.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.