SERBIA-KOSOVO-KARATE-MICHEZO

Wachezaji wa Karate wa Kosovo wapigwa marufuku kuingia Serbia

Viongozi wa Serbia wamezuia wachezaji wa Karate kutoka kosovo kuingi nchini humo.
Viongozi wa Serbia wamezuia wachezaji wa Karate kutoka kosovo kuingi nchini humo. Reuters/Antonio Bronic

Serikali ya Serbia imewazuia wachezaji wa mchezo wa Karate kutoka nchini Kosovo kuingia nchini humo ili kushiriki katika mashindano ya bara Ulaya.

Matangazo ya kibiashara

Sababu hizi zimelezwa kuwa ni za kisiasa, kwa sababu Serbia imekataa kutambua uhuru wa Kosovo uliofanyika mwaka 2008 na imeendelea kusisitiza kuwa Serbia na Kosovo ni nchi moja.

Mahusiano kati ya nchi hizo mbili yameendelea kuwa mabaya tangu miaka tisini.

Hii inaamana kuwa timu ya Kosovo itakosa michuano hiyo iliyoanza tangu Jumatano wiki hii na inatarajiwa kumaliza tarehe 13.