Kombe la Dunia 2018 kuchezwa Urusi

Michuano ya Kombe la Dunia inaanza kuchezwa Juni 14 hadi Julai 15, 2018.
Imehaririwa: 17/05/2018 - 07:42

Kombe la Dunia 2018, michuano ambayo itaanza Juni 14 hadi Julai 15. Kombe hilo la Dunia litashirikisha timu 32. Afrika inawakilishwa na Misri, Nigeria, Morocco, Tunisia na Senegal. Timu zimepangwa kwenye makundi kwa kufuata viwango vya soka vya FIFA mwezi Oktoba 2017. Kuna makundi manne, kila kundi likiwa na timu nne.