Pata taarifa kuu
CAF-TP MAZEMBE-KLABU BINGWA AFRIKA

TP Mazembe yachanua taji la klabu bingwa Afrika

TP Mazembe ilipochuana na Esperance ya Tunisia
TP Mazembe ilipochuana na Esperance ya Tunisia AFP
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Mabingwa mara tano wa taji la klabu bingwa Afrika TP Mazembe wameendlea na kampeni yao ya kusaka taji la klabu bingwa Afrika baada ya hapo jana kuirarua Difaa El Jadida ya Morocco kwa mabao 2-0.

Matangazo ya kibiashara

Kwa ushindi huo Mazembe imefikisha alama sita na kushikilia usukani wa Kundi B ambalo pia linajumuisha MC Alger na ES Setif za Algeria

Huo ni ushindi wa pili mfululizo wa Mazembe katika hatua ya makundi ya taji hilo baaada ya kupata ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya ES Setif ya Algeria katika mchezo wa kwanza.

Mabao ya Mazembe katika mchezo huo yalifungwa kipindi cha pili na Ben Malango na Abdoulaye Sissoko.

Mazembe sasa ina alama sita ikifuatiwa na MC Alger yenye alama nne wakati Jadida ina alama moja naa ES Setif inakamata mkiaa ikiwa bila alama yoyote.

Matokeo ya mechi nyingine…

KCCA ya Uganda iliwashinda maabingwa mara nane wa michuano hiyo Al Ahly ya Misri

Township Rollers ya Botswana ilifungwa mabao 4-1 na Esperance ya Tunisia

ES Setif ilifungwa bao 1-0 na MC Alger

Wydad Casablanca ambao ni mabingwa watetezi walipata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya AS Togo Ports

Mbabane Swallows ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Premiero Agosto ya Angola.

 

 

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.