Fifa-Ufaransa-Australia

Kundi C linatajwa kuwa na unafuu kwa Ufaransa

Kombe la Dunia
Kombe la Dunia FIFA.com

Kundi C linatajwa kuwa na unafuu kwa Timu ya Taifa ya Ufaransa, Le Blues

Matangazo ya kibiashara

Ufaransa, Australia, Peru na Denmark.

Ufaransa

Linatajwa kwanza ni kundi rahisi kwa Ufaransa maarufu kama Les Blues.Ufaransa inashika nafasi ya saba kwa ubora duniani kwa mujibu wa viwango vya Fifa.

Ufaransa imeshiriki fainali hizo mara 14, kufika nusu fainali mara mara tano, kufika fainali mara mbili na kutwaa ubingwa huo mara moja, mwaka 1998.

Didier Deschamp, nahodha wa kikosi kilichotwaa ubingwa 1998 na meneja wa zamani wa Monaco, Juventus na Marseille ndiye atakayeiongoza Ufaransa katika fainali hizo.

Nyota wa Ufaransa katika fainali za mwaka huu ni Antoine Griezman, alishinda tuzo ya mcheza bora na mfungaji bora wa michuano ya Euro 2016 na pia alifunga mabao manne na kusaidia upatikanaji wa mabao mengine manne katika mchakato wa kusaka tiketi ya kwenda nchini urussi.

Australia.

Inashika nafasi ya 40 kwa viwango vya ubora duniani.

Imeshiriki fainali hizo mara nne na mafanikio yao makubwa ni kucheza hatua ya 16 bora katika fainali zilizoandaaliwa na Ujerumani mwaka 2006.

Mholanzi, Bert Van Marwijk ndiye atakayekiongoza kikosi cha Australia katika fainali hizo, anakumbukwa kwa kuipeleka Uholanzi katika hatua ya fainali mwaka 2010 ambapo walifungwa na Hispania.

Awali aliiongoza Saudi Arabia kupata tiketi kabla ya kutimkia Australia. Ana uzoefu mkubwa na mashindano haya.

Tim Cahil ndiye mchezaji nyota katika kikosi hicho.

Peru

Imeshiriki fainali hizi mara nne na mafanikio makubwa ni kufika hatua ya robo fainali katika fainali za 1970 na 1978.

Gareca, mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Argentina ambaye lipewa jukumu la kuinoa timu hiyo mwaka 2015 , ataiongoza Peru katika fainali hizo.

Septemba 5, 2017 Peru iliifunga Ecuador mabao 2-1 na kupata tiketi ya kwenda kucheza mechi ya mtoani dhidi ya Newszealand kabala ya kupata tiketi ya kushiriki fainali hizo.

Jefferson Farfan ni mchezaji mwenye miaka 33 na ndiye nyota katika kikosi cha Peru.

Denmark

Imeshiriki fainali hizi mara 4 n mafanikio yao makubwa ni kufika hatua ya robo fainali mwaka 1998, fainali zilizoandaliwa na Ufaransa.

Hage Heraide atakiongoza kikosi cha Denmark baaada ya kuchukua mikoba ya Mrtin Olsen mwaka 2016.

Novemba 14, 2017, Denmark iliibamiza Ireland Kaskazini mabao 5-1 na kupata tiketi ya kushiriki fainali za mwaka huu.

Christian Eriksen ndiye mchezaji nyota katika kikosi cha Denmark.