ARSENAL-SOKA-MICHEZO

Emery apewa mikoba ya Wenger Arsenal

Meneja wa zamani wa Sevilla na PSG, Unai Emery, atangazwa kuwa meneja mpya wa Arsenal.
Meneja wa zamani wa Sevilla na PSG, Unai Emery, atangazwa kuwa meneja mpya wa Arsenal. Reuters

Klabu ya Arsenal kupitia afisa mkuu mtendaji wa klabu hiyo Ivan Gazidis imemtangaza Unai Emery, kuwa meneja mpya wa klabu hiyo kuchukua mikoba ya Arsene Wenger.

Matangazo ya kibiashara

Emery aliiachana na klabu yake ya PSG mwanzoni mwa mwezi huu na alikuwa jijini London, mapema wiki hii , kufanya mazungumzo na klabu ya Arsenal ya kuwa meneja mpya wa Gunners wa London.

Ataongoza Arsenal hadi kwenye enzi mpya baada ya kuondoka kwa Wenger, 68, aliyeshinda mataji matatu ya Ligi ya Premia na vikombe saba vya FA akiwa na klabu hiyo.

Meneja huyu raia wa Hispania, mwenye umri wa miaka 46,a liisaidia klabu ya PSG, kutwaa mataji matatu katika msimu uliomalizika katikati ya mwezi huu na nafasi yake katika miamba hao wa Ufaransa imechukuliwa na Thomas Tuchel.

Awali alikuwa meneja wa Sevilla ambapo aliwasaidia kushinda Europa League mara tatu mtawalia.

Kwa siku za hivi karibuni kiungo wa zamani wa Arsenal Mikel Arteta ndio alitajwa angepewa jukumu la kupewa kazi ya umeneja ya kuwaongoza Arsenal baada ya miaka 22, ya kuongozwa na Arsene Wenger.

Wakati huo huo kiungo wa Arsenal Santi Cazorla anaondoka klabuni hapo msimu huu baada ya kumalizika kwa mkataba wake, Cazorla ameichezea timu yake jumla ya michezo 180 toka alipojiunga na klabu hiyo mwaka 2012 akitokea Malaga.