REAL MADRID-LIVERPOOL-SOKA

Real Madrid na Liverpool kumenyana katika fainali ya UEFA

Kikkosi cha Real Madrid kitakutana kesho na Liverpool katika mchezo wa fainali ya UEFA.
Kikkosi cha Real Madrid kitakutana kesho na Liverpool katika mchezo wa fainali ya UEFA. REUTERS/Andrea Comas

Fainali ya Ligi ya mabingwa Ulaya, baina ya klabu ya Real Madrid na Liverpool itachezwa Jumamosi wiki hii katika Uwanja wa Olimpiki Mjini Kiev nchini Ukraine.

Matangazo ya kibiashara

Real Madrid inawania taji la tatu mfululizo la michuano hiyo wakati Liverpool inacheza fainali ya kwanza katika kipindi cha miaka 11.

Mara ya mwsiho Liverpool ilishinda taji hilo mwaka 2005 ilipoifunga AC Milan ya Italia kwa penati 3-2 baada ya timu hizo kufungana mabao 3-3 katika muda wa dakika 120.

Madrid wameshinda taji hilo mara 12, mara ya mwsiho walishinda taji hilo mwaka jana walipoifunga Juventus ya Italia kwa mabao 4-1. Liverpool imeshinda taji la Ulaya mara tano.

Liverpool imefunga jumla ya magoli 46 katika kampeni yao ya mashindano ya Ulaya msimu huu, wakati Reala Madrid ikitegemea zaidi huduma ya mshambuliaji wake Christiano

Ronaldo ambaye katika mchezo wa fainali dhidi ya Juventus alifunga mabao matatu kati ya manne yaliyofungwa na timu yake.

Fainali ya mwaka huu itakuwa ya 63 ya michuano ya Ulaya inayoandaliwa na shirikisho la kandanda barani humo, UEFA.