MICHEZO-TENISI

Serena Williams kuchuana na Kristyna Pliskov

Serena Williams anasema yuko tayari kutwaa ushindi.
Serena Williams anasema yuko tayari kutwaa ushindi. Reuters/Pascal Rossignol

Mshindi mara tatu wa taji la French Open, Serena Williams atachuana na Kristyna Pliskova wa Jamhuri ya Czech katika mechi ya mzunguko wa kwanza wa michuano hiyo ya tenisi ya French Open.

Matangazo ya kibiashara

Serena atashiriki taji la kwanza la Grand Slum tangu alipojifungua mtoto wa kike Septemba mwaka jana.

Mchezaji namba moja wa tenisi wa Uingereza Johana Konta atachuana na Yulia Putintseva kutoka Kazakhstan wakati mwingereza mwingine Kyle Edmund atachuana na raia wa Australia Alex de Minaur.

Michuano ya tenisi ya French Open inatazamiwa kuanza Juni Mei 27 na kutaamatika Juni 10.

Kwa upande wa wanaume Mshindi mara 16 wa grandslum, atakuwa mchezaji wa kuchungwa zaidi kwa upande wa wanaume.

Hata hivyo michuano ya mwaka itawakosa mshindi mara 20 Roger Federal na mwingereza, Andy Murray.

Uingereza itawakilishwa na wachezaji wawili, Kyle Edmund kwa uoande wa wanaume na Johana Konta kwa upande wa wanawake.