GHANA-RUSHWA-SOKA

Shirikisho la Soka nchini Ghana lavunjwa kutokana na tuhuma za rushwa

Kwesi Nyantakyi, rais wa Shirikisho la Soka la Ghana, anashtumiwa makosa kadhaa ya rushwa.
Kwesi Nyantakyi, rais wa Shirikisho la Soka la Ghana, anashtumiwa makosa kadhaa ya rushwa. Carl De Souza/AFP

Sintofahamu yaibuka nchini Ghana baada ya serikali kuchukua uamuzi wa kuvunja Shirikisho la Soka nchini humo kwa shutma za rushwa. Hili ni suala limezua wasiwasi miongoni mwa wadau wa soka nchini Ghana.

Matangazo ya kibiashara

Serikali kupitia wake Waziri wa Habari, Mustapha Abdul-Hamid, "imeamua kuchukua hatua za haraka kwa kulivunja kwa Shirikisho la Soka la Ghana" kwa sababu ya "shutma ya ya rushwa".

Uchunguzi wa siri uliofanywa na mwahabari kutoka Ghana Anas Aremeyaw Anas,uliweka wazi kashfa hiyo, na kuonesha namna ufisadi ulivyokithiri katika Shirikisho la soka nchini Ghana.

Huu ni uchunguzi ambao umemgusa pia rais wa Shirikisho la soka nchini humo Kwesi Nyantaki na waamuzi ambao wamekuwa wakipewa hongo ili kupendelea timu fulani.

Uchunguzi huu pia unamwonesha mwamuzi kutoka Kenya Aden Range Marwa, akipokea rushwa, madai ambayo amekanusha.

Anas ambaye amekuwa akichunguza suala hili kwa muda wa miaka miwili, sasa, amekuwa akipokea vitisho vya kuuawa.