FIFA-URUSI-KOMBE LA DUNIA 2018

Teknolojia ya VAR kuanza kutumiwa wakati wa mechi za kombe la dunia

Teknolojia ya VAR, itakayotumiwa wakati wa kombe la dunia nchini Urusi
Teknolojia ya VAR, itakayotumiwa wakati wa kombe la dunia nchini Urusi FIFA.COM

Kombe la dunia nchini Urusi, litashuhudia matumizi ya kwanza ya teknolojia ya Video Assistant Referee, mfumo wa video unaomwezesha mwamuzi kupitia ,kwa kutezama matukio mbalimbali yanayotokea uwanjani, wakati mechi ikiendelea.

Matangazo ya kibiashara

Shirikisho la soka duniani FIFA, limesema lengo la teknolojia hii ambayo tayari imeshafanyiwa majaribio hasa katika ligi za soka barani Ulaya, itasaidia kuleta ukweli na haki katika michuano hii.

Teknolojia hii itafanya vipi kazi ?

Jambo la kwanza ni kuwa teknolojia hii ya VAR, itatumiwa katika mechi zote 64 za kombe la dunia, kwa lengo la kutatua yafuatayo:-

-Kubaini iwapo goli limeingia na namna lilivyofungwa.

-Uamuzi wa kutoa mkwaju wa penalti, na sababu zilizosababisha hali hiyo kutokea.

-Iwapo mchezaji anastahili kupewa kadi nyekundu.

-Kuthibitisha jambo muhimu wakati wa mchezo huo.

Mwamuzi wa Kati kwa ushirikiano na maafisa wengine, watawasiliana ili kwenda kuthibitisha tukio fulani kupitia runinga, zitazokuwa zimetengwa katika eneo husika ili kurahihisha suala hili.