Pata taarifa kuu
KOMBE LA DUNIA-UFARANSA-AUSTRALIA

Ufaransa yawa ya kwanza kunufaika na teknolojia katika fainali za Kombe la Dunia

Paul Pogba akishangilia baada ya kuifungia Ufaransa bao la pili dhidi ya Australia katika fainali za Kombe la dunia Juni 16, 2018
Paul Pogba akishangilia baada ya kuifungia Ufaransa bao la pili dhidi ya Australia katika fainali za Kombe la dunia Juni 16, 2018 Sky Sports
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 1

Ufaransa imekuwa nchi ya kwanza inashoriki fainali za Kombe la dunia, imekuwa ya kwanza kunufaika na teknolojia ya video baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Australia.

Matangazo ya kibiashara

Mshambuliaji wa Ufaransa, Antoinne Griezman alichezewa madhambi katika eneo la hatari dakika ya 57 na mwamuzi Andres Cunha awali aliamua kuwa si penati lakini baada ya kupitia marudio ya video aliamuru upigwa mkwaju wa penati na Griezman akaandikia Ufaransa bao la uongozi.

Bao la pili la Ufaransa pia lilipatikana kupitia teknolojia ya mabao (goal line teknology) baada ya mpira uliopigwa na Paul Pogba kuvuka mstari kabla kuokolewa na kipa wa Australia.

Meneja wa Australia, Bert van Marwijk ameeleza kutoridhishwa na matokeo ya timu kwa sababu timu yake ilicheza vizuri kuliko wapinzani wao.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.