KOMBE LA KAGAME-CECAFA-SOKA

Gor Mahia na Simba zachanua, Kombe la Kagame

Katibu Mkuu wa Cecafa Nicholas Musonye
Katibu Mkuu wa Cecafa Nicholas Musonye Kismaayodaily.com

Simba na Gor Mahia zimefuzu hatua ya nusu fainali ya Kombe la Kgame baada ya kushinda mechi zao za jana.

Matangazo ya kibiashara

Gor Mahia iliilaza Vipers mabao 2-1 wakati Simba iliishinda AS Sports ya Djibout kwa bao 1-0 lililofungwa na Mohammed Rashid.

Kwa matokeo hayo Simbaa inasubiri mshindi wa mchezo baina ya Rayon Sports na Azam zinazochuana leo wakati Gor Mahia watakabiliana na ama Singida United ama JKU.

Michuano hiyo itaafikia tamati Julai 13 kwa mchezo wa fainali utaakaochezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.