SOKA-REAL MADRID-JUVENTUS

Miaka tisa ya Ronaldo katika Uwanja wa Santiago Bernabeu yatamatika rasmi

Christiano Ronaldo wakati huo akiwa mchezaji wa Real Madrid
Christiano Ronaldo wakati huo akiwa mchezaji wa Real Madrid Reuters/Massimo Pinca

Mshambuliaji Christiano Ronaldo ameachana rasmi na klabu ya Real Madrid na kujiunga na klabu ya Juventus ya Italia kwa ada ya uhamisho wa Euro milioni 105.

Matangazo ya kibiashara

Ronaldo alijiunga na Real Madrid mwaka 2009 kwa ada iliyovunja rekodi ya pauni milioni 80, akitokea Manchester united ya England.

Usajili huu umekamilishwa hivi leo baada ya juhudi kubwa zilizofanywa na rais wa Juventus Andrea Agnel. Real Madrid pia imethibitisha kupitia ukurasa wake katika mtandao wa Instagram kuondoka kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno.

Akiwa nchini Hispania Ronaldo ameshinda mataji mawili ya La Liga, mataji manne ya Ligi ya mabingwa Ulaya na kombe la mfalme.