SOKA-REAL MADRID-JUVENTUS

Uhamisho wa Ronaldo huenda ukakamilika saa 48 zijazo

Mshambuliaji wa Real Madrid Christiano Ronaldo akifunga bao katika mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya, msimu uliopita
Mshambuliaji wa Real Madrid Christiano Ronaldo akifunga bao katika mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya, msimu uliopita Alberto PIZZOLI / AFP

Ripoti kutoka nchini Italia zinasema usajili wa mshambuliaji Christiano Ronaldo kutoka Real Madrid kwenda Juventus huenda ukakamilika saa 48 zijazo.

Matangazo ya kibiashara

Habari zilizochapishwa na Sky Sports zinasema wakala wa mchezaji huyo, George Mendes leo jumanne anakutaana na rais wa Real Madrid Florentino Perez kujadili hatima ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33.

Juventus inapanga kutumia euro milioni 88 ili kukamilisha usajili wa mchezaji huyo, mshindi mara tano wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia.