UFARANSA-UBELGIJI-SOKA

Kombe la Dunia 2018: Les Blues wafurahia ushindi wao dhidi ya Ubelgiji

Didier Deschamps, aliyewahi kuwa bingwa wa dunia kama mchezaji, anatarajia kuwa bingwa wa dunia kama kocha, ikiwa vijana wake watafaulu kushinda mechi ya fainali ya Kombe la Dunia 2018, Urusi.
Didier Deschamps, aliyewahi kuwa bingwa wa dunia kama mchezaji, anatarajia kuwa bingwa wa dunia kama kocha, ikiwa vijana wake watafaulu kushinda mechi ya fainali ya Kombe la Dunia 2018, Urusi. Reuters

Timu ya taifa ya Ufaransa, Les Bleus imetinga fainali za Kombe la Dunia kwa mara ya tatu katika historia yake baada ya kuilaza Ubelgiji (1-0) Jumanne hii Julai 10 katika uwanja wa St Petersburg. Bao la Ufaransa lilifungwa na Samuel Umtiti.

Matangazo ya kibiashara

Vijana wa Didier Deschamps watajitupa uwanjani Jumapili Julai 15, dhidi ya mshindi kati ya Uingereza na Croatia.

Mabingwa wa Dunia 1998 Ufaransa waliendeleza fomu yao nzuri nchini Urusi kwa kuiadhibu timu ya Ubelgiji kupitia bao la Samuel Umtiti katika dakika ya 50.

Kylian Mbappe, ambaye alikua hajazaliwa wakati timu ya taifa ya Ufaransa ilipotwaa ubingwa wa Kombe la Dunia 1998, ni mmoja wa wachezaji waliochangia pakubwa ushindi huo.

Ubelgiji ilikuwa na Eden Hazard na mchezaji wa Chelsea ambaye alicheza vizuri katika kipindi cha kwanza cha mchezo bila hata hivyo kufanya maajabu upande wa "Les Bleus".

Kufikia sasa Ufaransa imefungwa tu mabao manne ikiwa ni pamoja na mabao matatu dhidi ya Argentina na moja dhidi ya Australia.

Hata hivyo, Ubelgiji itacheza Jumamosi tarehe 14 Julai kuwania nafasi ya tatu ugani Krestovsky.

Ni mara ya tatu Ufaransa kutua fainali na mafaniko hayo yamekuwa ni nafuu kwani ilikuwa ni jaribio lao la saba.