SOKA-KOMBE LA DUNIA-GIAN INFANTINO

Fainali za Kombe la dunia 2022 kupigwa mwezi Novemba hadi Disemba

Rais wa Shirikisho la kandanda duniani, Fifa, Gian Infantino
Rais wa Shirikisho la kandanda duniani, Fifa, Gian Infantino REUTERS/Sergei Karpukhin

Shirikisho la kandanda duniani Fifa limesema kwamba fainali za Kombe la dunia za mwaka 2022 nchini Qatar zitachezwa mwezi wa Novemba hadi Disemba.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Shirikisho la kandanda duniani Fifa, Gian Infantino ametoa matamshi hayo wakati akizungumza mafanikio ya Urusi katika kuandaa fainali za kombe la dunia za mwaka huu ambazo zitafikia tamati kesho.

Kwa mujibu wa infantino fainali hizo zitachezwa kutoka Novemba 21 hadi Disemba 18 nchini Qatar.

Aidha Infantino amepongeza maandalizi ya Urusi yaliyopelekea kufanikisha fainali za mwaka huu.

"Pongezi ziende kwa serikali, shirikisho la soka na wadau wengine wa kujitolea waliofanikisha michuano ya mwaka huu,"