CECAFA-KOMBE LA KAGAME-GOR MAHIA

Gor Mahia yafungiwa miaka miwili kushiriki michuano ya Cecafa

Wachezaji wa Gor Mahia wakishangilia baada ya kushinda taji la Sport Pesa kwa kuifunga Simba mabao 2-0
Wachezaji wa Gor Mahia wakishangilia baada ya kushinda taji la Sport Pesa kwa kuifunga Simba mabao 2-0 Twitter/Sport Pesa

Gor Mahia imefungiwa kushiriki michuano ya Cecafa inayoandaliwa na shirikisho la Kandanda Afrika Mashariki na Kati, Cecafa kutokana na vitendo vya utovu wa nidhamu vilivyoonyeshwa na wachezaji wake.

Matangazo ya kibiashara

Gazeti la The Standard la Kenya, limearifu

Uamuzi huo,umefikiwa baada ya kikao cha kamati ya utendaji ya Cecafa kilichoketi Jijini Dar es Salaam baada ya timu hiyo kukataa kupokea zawadi ya mshindi wa tatu.

Pia Cecafa kupitia katibu mkuu Nicholaus Musonye, mbali naa kuipoka medali ya ushindi wa tatu pia Cecafa imeagizi shirikisho la soka Kenyaa kumchukulia hatua kocha wa Gor Mahia Dylan Kerr kutokana na matamshi yake machafu kwa waamuzi.