Pata taarifa kuu
KOMBE LA DUNIA-CROATIA-UFARANSA

Mfahamu mwamuzi Nestor Pitana atakayechezesha fainali ya Croatia na Ufaransa

Nestory Pitana, mwamuzi atakayechezesha fainali ya kombe la dunia baina ya Croatia na Ufaransa
Nestory Pitana, mwamuzi atakayechezesha fainali ya kombe la dunia baina ya Croatia na Ufaransa FIFA.COM
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Je, unamfahamu mwamuzi Nestor Pitana kutoka Argentina atakayechezesha fainali ya kombe la dunia baina ya Croatia na Ufaransa.Amekuwa mwamuzi wa kimataifa mwenye beji ya Fifa tangu mwaka 2010 na ni miongoni mwa waamuzi wenye uzoefu mkubwa kutoka Amerika kusini.Mwamuzi huyu ana umri wa miaka 43 na ndiye aliyechezesha mechi ya ufunguzi wa fainali hizo, Juni 14 baina ya wenyeji Urusi na Saudi Arabia ambapo Urusi walishinda mabao 5-0.Alichezesha fainali za kombe la dunia za vijana chini ya miaka 17 mwaka 2013 na pia alichezesha fainali za kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil, miongoni mwa mechi alizochezesha ni ile ya robo fainali baina ya Ufaransa na Ujerumani.Ni mwamuzi wa pili kutoka Argentina kuchezesha fainali ya kombe la dunia, Horacio Elizondo muargentina mwingine alichezesha fainali ya mwaka 2006 baina ya Italia na Ufaransa.  

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.