Pata taarifa kuu
KOMBE LA DUNIA-UFARANSA-CROATIA

Ufahamu Uwanja utakaochezewa fainali ya Kombe la dunia

Uwanja wa Luzhniki utakaoandaa mechi ya ufunguzi na fainali ya Kombe la Dunia
Uwanja wa Luzhniki utakaoandaa mechi ya ufunguzi na fainali ya Kombe la Dunia FIFA.COM
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Mamilioni ya wapenda soka dunia wanasubiri kwa hamu na ghamu kushuhudia mchezo wa fainali ya kombe la dunia baina ya Croatia na Ufaransa lakini je unaufahamu Uwanja wa Luzhniki, utakaotumika katika mchezo huo?

Matangazo ya kibiashara

Uwanja huu una uwezo wa kuchukua watazamaji 81,000 na ni miongoni mwa viwnaja vikubwa vya soka barani Ulaya.

Uwanja huu unamilikiwa na serikali ya Urusi na unapatikana katika Wilaya ya Khamovniki Moscow, Urusi.

Uwanja huu, ulikuwa mojawapo ya miundombinu iliyotumiwa wakati wa michuano ya Olimpiki ya mwaka 1980.

Mara mbili, uwanja huu umeandaa fainali ya Ligi ya mabingwa Ulaya mwaka 1999 ambapo Manchester United ilichuana na Bayern Munich na mwaka 2008 ambapo Manchester united ilichuana na Chelsea.

Endelea kufuatilia mtandao wetu kwa habari kemkemu kuelekea kutamatika kwa fainali za Kombe la dunia

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.