Kenya imekuwa nchi bora katika mashindano ya riadha ya Afrika baada ya kunyakua medali 19, zikiwemo 11 za dhahabu, ikifuatwa na Afrika Kusini na wenyeji Nigeria. Yalikuwa ni mashindano ya 21, yaliyoshuhudia maandalizi mabaya yaliyosababisha mamia ya wanariadha kukwama katika uwanja wa ndege mjini Lagos baada ya kukosa ndege ya kuwapeleka mjini Asaba. Tanzania nayo ilijiondoa. Tunajadili.