TANZANIA-SOKA-SIMBA SC

Simba yarejea Tanzania baada ya kumaliza kambi ya maandalizi, Uturuki

Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba SC wanarejea nyumbanibaada ya kukamilisha kambi ya maandalizi nchini Uturuki.

Kikosi cha Simba
Kikosi cha Simba Global publishers
Matangazo ya kibiashara

Simba ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara wanakabiliwa na mashindano mbalimbali msimu ujao, ikiwemo Ligi Kuu ambayo itaanza Agosti, 22.

Ikiwa nchini Uturuki Simba ilichezwa mechi mbili za kirafiki, ikitoka sare mchezo mmoja na kushinda mchezo mmoja.

Simba inarejea nchini Tanzania, siku tatu kabla ya tamasha la Simba day ambalo hufanyika kila mwaka, katika tamasha la mwaka huu Simba itakuwa inatimiza miaka 82 tangu kuanzishwa kwake.

Mashindano mengine ni Kombe la Shirikisho nchini Tanzania, Klabu bingwa barani Afrika, Michuano ya Kombe la Mapinduzi na michuano ya Spprts Pesa ambayo huandaliwa kila mwaka kwa klabu zinazodhaminiwa na kampuni ya Sports Pesa,ikishirikisha timu kutoka Tanzania na Kenya.

Aidha, mashabiki wa Simba watapata kutambulishwa wachezaji wapya waliosajiliwa na klabu hiyo kuelekea msimu ujao, akiwemo mshambuliaji meddy Kagere ambaye alinunuliwa kutoka klabu ya Gor Mahia ya Kenya