MISRI-SOKA-KOMBE LA DUNIA

Essam El-Haddary astaafu kucheza soka kwa mafanikio lukuki

Kipa na nahodha wa Misri Essam El Hadary mwenye umri wa miaka 45
Kipa na nahodha wa Misri Essam El Hadary mwenye umri wa miaka 45 FIFA.COM

Mlinda mlango wa kimataifa wa Misri, Essam El Hadary ametangaza kustaafu soka la kimataifa, miezi miwili baada ya kuweka rekodi ya kuwa mchezaji mchezaji mwenye umri miubwa kuwahi kucheza fainali za Kombe la dunia.

Matangazo ya kibiashara

El Hadary, alikuwemo kwenye kikosi cha Misri kilichoshiriki fainali za Kombe la dunia nchini Urusi.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 45 anastaafu kucheza soka la kimataifa akiwa ameitumikia Timu ya Taifa ya misri, michezo 159 na kushinda mataji manne ya mataifa ya Afrika na pia akiwa ameifungia nchi yake bao moja.

Aidha meweka rekodi ya kuwa mchezaji mkongwe kuokoa penati katika fainali za kombe la dunia, alicheza mkwaju wa penati katika mchezo wa mwisho wa kundi A baina ya Misri na Saudi Arabia.