TANZANIA-SOKA-SIMBA SC

Simba kuikabili Asante Kotoko, ikiadhimisha miaka 82 ya uhai wake

Wachezaji wa Simba katika Utambulisho wa jezi mpya zitakazotumika msimu ujao
Wachezaji wa Simba katika Utambulisho wa jezi mpya zitakazotumika msimu ujao Instagram/Simba Sports Club

Mabingwa wa soka Tanzania, Simba kesho watachuana na Asante Kotoka ya Ghana katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki utakaochezwa kesho Agosti nane katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Matangazo ya kibiashara

Mchezo huo utakuwa sehemu ya sherehe za klabu ya Simba kutimiza miaka 82 tangu ilipoasisiwa mwaka 1936. Pia Simba itatumia siku hiyo kutambulisha wachezaji wake waliosajiliwakwa msimu ujao wa michuano ya Ligi Kuu na ile ya kimataifa.

Kueleke mchezo huo, Simba inayojivunia uwekezaji wa Mfanyabiashara Mohammed Dewji, iliweka kambi ya wiki mbili nchini Uturuki sanjari na kucheza mechi mbili za kujipima uwezo.

Mbali na mcgezo huo pia burudani mbalimbali za muziki ikiwemo Bendi maarufu ya Twanga pepeta watashiriki kutoa burudani kwa mashabiki watakaofika uwanja wa Taifa kushuhudia tukio hilo.