RWANDA-SOKA-RAYON SPORTS

Usengimana asajiliwa na klabu ya Al-Khaitan ya Kuwait

Faustine Usengiwmana
Faustine Usengiwmana www.newtimes.co.rw

Klabu ya Al-Khaitan SC ya Kuwait imekamilisha usajili wa beki wa kimataifa wa Rwanda, Fautin Usengimana.

Matangazo ya kibiashara

Mchezaji huyo ambaye pia anaichezea Timu ya Taifa ya Rwanda, amesaini mkataba wa miaka miwili baada ya kumaliza mkataba wake na klabu ya Rayon Sports ya Rwanda.

Akizungumza na gazeti la New Times la Rwanda mchezaji huyo amesema anajisikia faraja kuanza maisha mapya ya kisoka katika taifa hilo la Asia.

“Hii ni fursa adhimu kwangu kama mchezaji na ninatumai kuitumia kikamilifu kusonga mbele,”amearifu mchezaji huyo.

Usengimana alikuwemoe kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Rwanda chini ya miaka 17 kilichocheza fainali za Afrika mwaka 2011 na pia alikuwemo kwenye kikosi cha vijana kilichoshiriki fainali za kombe la dunia mwaka huohuo nchini Mexico.