BARCELONA-MANCHESTER UNITED-PAUL POGBA

Wakala wa Paul Pogba afikiria kumuuza mchezaji huyo Barcelona

Wakala wa kiungo wa Manchester United na Timu ya Taifa ya Ufaransa ametoa matamshi ya kushangaza kuwa ana mpango wa kumuuza mchezaji huyo katika klabu ya Barcelona ya Hispania.

Paul pogba akishika Kombe la dunia baada ya Ufaransa kuishinda Croatia mwezi juni nchini Urusi
Paul pogba akishika Kombe la dunia baada ya Ufaransa kuishinda Croatia mwezi juni nchini Urusi REUTERS/Michael Dalder
Matangazo ya kibiashara

Pogba alitoa mchango mkubwa kwa Ufaransa iliposhinda fainali za Kombe la dunia Mwezi juni nchini Urusi na ripoti zinasema licha mchezaji huyo kurejea katika klabu yake ya Manchester United, hana maelewano mazuri na Kocha Jose Mourinho.

Gazeti la Daily mail la nchini Uingereza limefichua kuwepo kwa mpango huo na kwamba wakala Mino Raiola yu kwenye mipango ya kuhakikisha mteja wake anahamia Barcelona kabla ya kutamatika kwa dirisha la majira ya joto.

Mwaka 2016, Raiola alifanikisha kumhamisha Pogba kutoka Juventus kwenda Manchester United kwa dau la Euro milioni 89.

Endapo,Pogba ataihama United, itakuwa pigo kwa Jose Mourihno ambaye mpaaka sasa anailaumu bodi ya Manchester United kwa kushindwa kutoa fedha za usajili wa wachezaji wapya.

Dirisha la usajili nchini England linafungwa Alhamisi,Agosti 9 wakati mataifa mengine ya Ulaya yataendelea na usajili hadi mwishoni mwa mwezi wa Agosti.