KENYA-RIADHA-MICHEZO

Wanariadha wa Kenya walakiwa kwa vifijo na nderemo

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta akikabidhi bendera ya Kenya kwa wanariadha na wanamichezo wa nchi hiyo wanaoenda kushiriki michezi ya Olimpiki ya Rio, 22 Julai 2016
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta akikabidhi bendera ya Kenya kwa wanariadha na wanamichezo wa nchi hiyo wanaoenda kushiriki michezi ya Olimpiki ya Rio, 22 Julai 2016 Kenya Government

Wanariadha wa Kenya waliokuwa wa kwanza katika mashindano yaliyokamilika Jumapili iliyopita, nchini Nigeria wamerejea nyumbani. Serikali ya Kenya imeelezea furaha yake kwa matokeo hayo mazuri .

Matangazo ya kibiashara

Waliwasili jijini Nairobi, na kulakiwa kwa vifijo na nderemo na maafisa wa serikali na ndugu zao katika uwanja wa ndege za Kimataifa wa Jomo Kenyatta.

Licha ya mazingira magumu waliyokabiliana nayo kuelekea katika mashindano hayo ikiwa ni pamoja na kukosa ndege kutoka Lagos kwenda mjini Asaba, Kenya ilimaliza ya kwanza kwa medali 19 zikiwemo 11 za dhahabu.

Serikali ya Kenya, ikiongozwa na rais Uhuru Kenyatta imesema imefurahishwa sana na matokeo hayo mazuri yanayoonesha kuwa Kenya inasalia makao makuu ya mchezo wa riadha barani Afrika na duniani.