BURUNDI-FIFA-SOKA

Saido Berahino aruhusiwa kujiunga na timu yake ya taifa

Mshambuliaji wa klabu ya Stoke City nchini Uingerenze, Mrundi Saido Berahino amepewa idhini ya kuichezea timu yake ya taifa. Uamuzi huu umetolewa na Shirikisho la soka duniani FIFA.

Kikosi cha timu ya taifa ya Burundi Intamba mu Rugamba.
Kikosi cha timu ya taifa ya Burundi Intamba mu Rugamba. RFI-KISWAHILI
Matangazo ya kibiashara

Berahino mwenye umri w amiaka 25, ni raia wa Uingereza ana amewahi kuchezea timu ya taufa ya vijana wasioizidi miaka 16 na 21.

Hata kabla ya uamuzi huu wa FIFA, Shirikisho la soka nchini Burundi limekuwa likimwomba aiichezea timu ya taifa, bila mafanikio.

Iwapo atakubali kwenda kucheza nyumbani, ataichezea Intamba Murugamba katika mechi muhimu ya kufuzu kucheza fainali ya Afrika mwaka ujao nchini Cameroon.