MICHEZO-TENISI

Serena Williams ajiondoa katika mashindano ya Roger Cup

Serena Williams, Bingwa wa mataji makubwa 23 amesema hatashiriki mashindano ya Roger Cup kwa sababu zake kibinafasi
Serena Williams, Bingwa wa mataji makubwa 23 amesema hatashiriki mashindano ya Roger Cup kwa sababu zake kibinafasi REUTERS/Christian Hartmann

Mchezaji wa mchezo wa Tennis kutoka Marekani Serena Williams amesema amejiondoa katika mashindano ya Roger Cup nchini Canda, baada ya kujitafakari na kuona kuwa, akienda kushiriki hatakuwa mama mzuri kwa mtoto wake.

Matangazo ya kibiashara

Bingwa huyo wa mataji makubwa 23 amesema hatashiriki kwa sababu za kibinafasi.

Serena mwenye umri wa miaka 36, alijifunguia mwaka 2017, na amekuwa akirejea katika mchezo huu na mwezi Julai alifika katika fainali ya kuwania taji la Wimbledon huko Uingereza.

Wiki iliyopita, alipata matokeo mabaya baadsa ya kucharazwa na Mwingereza kwa seti za 6-1, 6-0 katika mashindano ya Silicon Valley clkassic huko Marekani