USAJILI-CHELSEA-LIVERPOOL-UINGEREZA

Dirisha la uhamisho wa wachezaji kufungwa leo nchini Uingereza

Mateo Kovacic amejiunga na klabu ya Chelsea kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea real Madrid
Mateo Kovacic amejiunga na klabu ya Chelsea kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea real Madrid Instagram/mateokovacic8

Dirisha la uhamisho wa wachezaji katika majira ya joto linafungwa leo nchini Uingereza huku Chelsea ikiwa imeweka rekodi ya uhamisho ghali zaidi wa golikipa duniani.

Matangazo ya kibiashara

Ada ya Euro milioni 71 kwa golikipa Kepa Arrizabalaga kutoka klabu ya Athletic Bilbao ya Hispania, uajili huo unakuja baada ya Chelsea kuondokewa na golikipa wake Thibaut Courtois aliyejiunga na klabu ya Real Madrid ya Hispania kwa ada ya Euro milioni 35.

Aidha Chelsea imemsajili kwa mkopo wa mwaka mmoja kiungo Matteo Kovacic kutoka Real Madrid.

Awali, Liverpool ilimsajili kipa Allison kutoka AS Roma kwa ada ya Euro milioni 66.

Manchester United inahaha kusaka wachezaji nyota kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili na ripoti za hivi punde zinasema inazungumza na beki wa Atletico Madrid Diego Godin ili kumpeleka Old Trafford.