SOKA-SIMBA-ASANTE KOTOKO

Djuma:Simba itatoa ushindani michuano ya CAF

Wachezaji wa SImba wakisherehekea ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Yanga katika mchuano muhimu wa taji kuu Tanzania bara
Wachezaji wa SImba wakisherehekea ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Yanga katika mchuano muhimu wa taji kuu Tanzania bara Goal.com

Kocha Msaidizi wa klabu ya Simba, Masoud Djuma ametoa ufafanuzi baada ya klabu hiyo kutoka sare ya bao 1-1 na Asante Kotoko ya Ghana katika mchuano wa kimataifa wa kirafiki.

Matangazo ya kibiashara

Djuma, raia wa Burundi ameiambia RFI Kiswahili kwamba Simba imepata maaandalizi kabambe na benchi la ufundi litatumia siku zilizobaki kufanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu.

“Hii mechi ilikuwa muhimu kwetu, na zaidi tumeutumia kujifunga na kuelewa wapi tufanyie kazi. Simba imesajili wachezaji wengi, wanahitaji muda ili kucheza pamoja.

Katika mchezo huo Simba ililazimika kusawazisha bao dakika ya 75 kupitia Emanuel Okwi baada ya kufungwa kipindi cha kwanza kwa bao la Michael Yeboah.

Simba ilicheza na Asante Kotoko kwa mara ya kwanza, mara ya mwisho timu hizo zilikutana nchini Kenya mwaka 2004 kwenye michuano ya Tusker ambapo Simba ilishinda mabao 4-2.

Simba itaingia kambini kujiandaa na mchezo wa ngao ya jamii dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezwa Agosti 18 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Jijini Mwanza.