UINGEREZA-SOKA

Dirisha kuu la usajili wa wachezaji lafungwa Uingereza

Klabu zinazocheza ligi nyingine England na Wales, ikiwa ni pamoja na ligi za Championship, League One na League Two bado zinaweza kuendelea kuwanunua wachezaji hadi mwisho wa mwezi huu.
Klabu zinazocheza ligi nyingine England na Wales, ikiwa ni pamoja na ligi za Championship, League One na League Two bado zinaweza kuendelea kuwanunua wachezaji hadi mwisho wa mwezi huu. REUTERS

Klabu za Everton na Fulham na Lecester City nchini Uingereza, walifanya usajili mkubwa lakini kwa mara ya kwanza katika historia ya ligi kuu ya soka nchini humo, kiwango kilichotumiwa kusajili wachezaji wapya kilipungua kwa Pauni Bilioni 1.2 ndani ya miaka minane.

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Alhamisi ilikuwa siku ya mwisho ya kuwasajili wachezaji.

Tottehnham Hotspurs ndio klabu pekee ambayo haikumsajili mchezaji yeyote msimu huu.

Usajili mkubwa hata hivyo umekuwa ni kwa Everton ambayo imemnunua mchezaji Yerry Mina kutoka Barcelona kwa Pauni Milioni 27.

Klabu zinazocheza ligi nyingine England na Wales, miongoni mwake ligi za Championship, League One na League Two bado zinaweza kuendelea kuwanunua wachezaji hadi mwisho wa mwezi huu.

Soko la kuhama wachezaji Scotland pia litafungwa 31 Agosti sawa na katika mataifa mengine Ulaya.