SOKA-LIGI KUU YA UINGEREZA-MANCHESTER UNITED

Ligi Kuu ya Uingereza yaanza kutimua vumbi

Nyota wa Manchester United, Alexis Sanchez anatajwa kuwa miongoni mwa  wachezaji watakaoibeba timu hiyo msimu huu
Nyota wa Manchester United, Alexis Sanchez anatajwa kuwa miongoni mwa wachezaji watakaoibeba timu hiyo msimu huu REUTERS/Scott Heppell

Ligi Kuu ya soka nchini England inaanza kutimua vumbi leo ambapo mashetani wekundu Manchester United itachuana na Leicester City, majira ya saa nne kwa saa za Afrika Mashariki.

Matangazo ya kibiashara

Mabingwa mara 20, United, waanza kampeni ya kuwania taji huku meneja wake Jose Mourihno akilalama kutokana na klabu hiyo kushindwa kufanya usajili mkubwa majira haya ya joto.

Dirisha la usajili nchini humo lilitamatika jana huku Manchester United ikiwa imefanya usajili wa mchezaji mmoja, Mbrazil Fred kwa dau la Uero milioni 50.

Mechi za kesho Jumamosi

Newcastle itachuana na Tottenham Hotspurs

Fulham itachuana na Crystal Palace

Huddesfield itakabiliana na Chelsea

Bounermouth itapambana na Cardiff City

Watford itapambana na Brighton