SOKA-UFARANSA-LIGI KUU

Msimu wa 81 wa Ligi Kuu ya Ufaransa waanza

Ligi Kuu ya Ufaransa inaanza kuunguruma leo kwa mchezo mmoja ambao utazikutanisha Olympique Marseille dhidi ya Tolouse.

PSG ndio mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Ufaransa
PSG ndio mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Ufaransa FRANCK FIFE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kesho Jumamosi kutakuwa na michezo mingine ambapo Nantes vs Monaco, Angers itachuana na Nimes, Lille itapambaana na Rennes, Montpellier itachuana na Dijon, Nice itapambana na Reims.

Jumapili pia kutakuwa na michezo mbalimbali ambapo mabingwa watetezi wa ligi hiyo Paris Saint Germain itakumbana na Caen, Bordeaux itakuwa mwenyeji wa Strasbourg na Olympique Lyonnais itachuana na Amiens Sports Club.

Ligi Kuu ya Ufaransa itafikia tamati Mei mwakani.