UEFA-REAL MADRID-ATHLETICO MADRID

Real Madrid na Athletico Madrid kuwania taji la UEFA Super Cup

Nembo ya UEFA
Nembo ya UEFA REUTERS/Jean Pierre Amet

Klabu za Uhispania, Real Madrid na Athletico Madrid zinakutana katika fainali ya kuwania taji la 43 la UEFA Super Cup inayochezwa Jumatano usiku katika uwanja wa Lillekula mjini Talinn nchini Estonia.

Matangazo ya kibiashara

Fainali ya taji hili, huandaliwa kila mwaka, kati ya bingwa wa taji la klabu bingwa barani Ulaya na Europa league.

Mechi hii itachezwa kuanzia saa nne usiku saa za Afrika Mashariki. Hii ndio fainali ya kwanza kuwahi kufanyika nchini Estonia.

Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA mwezi Machi, lilikubali kuwa iwapo mechi hii itachezwa katika muda wa ziada basi mchezaji wa azidi aruhusiwe kuingia na hivyo, kufanya wachezaji wa ziada katika mechi hii kuwa wanne.

Hii ni mara ya tano kwa klabu kutoka Uhispania, kucheza katika fainali hii kubwa barani Ulaya.

Real Madrid wanakwenda katika mchuano huu bila ua mshambuliaji wake wa zamani Christiano Ronaldo, huku kocha Julen Lopetegui akiongoza kikosi hicho kwa mara ya kwanza baada ya kujiuzulu kwa Zinedine Zidane.

Naye kocha wa Athletico Madrid, Diego Simeone atakuwa nje ya uwanja wakati wa mechi hii baada ya kufungiwa mechi nne wakati wa mchuano wa nusu fainali dhidi ya Arsenal.

Iwapo Real Madrid watashinda taji hili, watakuwa mabingwa mara tatu mfululizo. Klabu hii imeshinda mataji 23 katika makala 42 yaliyoshinda.