FIFA-SOKA-UBORA

FIFA: Senegal na Tunisia timu bora barani Afrika

Senegal na Tunisia zinaongoza katika ubora wa mchezo wa soka barani Afrika baada ya Shirikisho la soka duniani FIFA, kutangaza viwango vya ubora wa nchi mbalimbali mwezi huu.

Nembo ya Shirikisho la soka duniani FIFA
Nembo ya Shirikisho la soka duniani FIFA AFP PHOTO / FABRICE COFFRINI
Matangazo ya kibiashara

Licha ya kuongoza Afrika, Tunisia imeshuka nafasi tatu huku Senegal nayo ikipanda nafasi 24 duniani.

Misri imeshuka, nafasi 20 na sasa ni ya 65 duniani, baada ya matokeo mabaya katika michuano ya kombe la dunia mwezi Julai nchini Urusi.

Barani Afrika, Misri inashikilia nafasi ya 11.

Duniani, Ufaransa ndio nchi bora katika mchezo huu, baada ya kunyakua kombe la dunia, na imechukua nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Ubelgiji ambayo kwa sasa ni ya pili, huku Brazil ikiwa ya tatu.

DRC inaongoza katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na 37 duniani.

Uganda ni ya kwanza katika Ukanda wa CECAFA, na ya 17 barani Afrika, na 82 duniani, ikifuatwa na Kenya ambayo ni ya 112.

Rwanda inashikilia nafasi 136, Tanzania 140, Burundi 148, Ethiopia 151 na Sudan Kuisni ikiwa ya 156.

Somalia ni ya mwisho duniani ikiwa katika alama 206, pamoja na Eritrea, Tonga na Bahamas.

Timu bora barani Afrika, lakini nafasi ya dunia kwenye mabano:

1.Tunisia (24)

1.Senegal (24)

3.DR Congo (37)

4.Ghana (45)

5.Morocco (46)

6.Cameroon (47)

7.Nigeria (49)

8.Burkina Faso (52)

9.Mali (63)

10.Cape Verde Islands (64)