EVERTON-SOKA-GOR MAHIA
Everton kuchuana na Gor Mahia mwezi Novemba
Imechapishwa:
Everton ya Uingereza itaipokea Gor Mahia katika mchuano wa Sports Pesa utakaochezwa mwezi Novemba katika Uwanja w a Goodson Park.
Matangazo ya kibiashara
Mchezo huo utakuwa maalumu kwa kuwa nia taji la Sports Pesa. Gor Mahia ilipata nafasi ya kuchuana na Everton baada ya kuishinda Simba SC ya Tanzania kwa mabao 2-0.
Awali, mchezo huo ulipangwa kuchezwa mwezi Julai lakini umesogezwa mbele kutokana na sababu mbalimbali.
Everton na Gor Mahia zote zinadhaminiwa na kampuni ya Sports Pesa.