SOKA-ITALIA-CHRISTIANO RONALDO

Ligi Kuu ya Italia kuanza kesho

Ligi Kuu ya soka nchini Italia inatazamiwa kuanza kesho huku mabingwa watetezi Juventus wakitazamiwa kuchuana na Chievo Verona.

Mshambuliaji Christiano Ronaldo anatazamiwa kuanza kuitumikia klabu yake ya mpya ya Juventus
Mshambuliaji Christiano Ronaldo anatazamiwa kuanza kuitumikia klabu yake ya mpya ya Juventus REUTERS/Massimo Pinca
Matangazo ya kibiashara

Ligi hiyo inaelekea kuanza huku Juventus ikipewa nafasi kubwa ya kufanya vyema baada ya kumsajili mshambuliaji Christiano Ronaldo kutoka Real Madrid.

Mechi nyingine itakayochezwa kesho ni baina ya Lazio na Napoli.

Jumapili pia kutakuwa na michezo kadhaa ambapo Torino itachuana na Roma, Empoli itaipokea Cagliari, Bologna itachuana na Spal, Parma itachuana na Udenese.