SOKA-TANZANIA-SIMBA SC

Ligi ya Tanzania kuanza bila mdhamini mkuu

Ligi Kuu ya Tanzania Bara inatazamiwa kuanza Agosti 22
Ligi Kuu ya Tanzania Bara inatazamiwa kuanza Agosti 22 AzaniaPost

Ligi Kuu ya Tanzania Bara inatazamiwa kuanza wiki ijayo bila kuwa na mdhamini mkuu wa ligi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mantiki hiyo, klabu zitakazoshiriki ligi hiyo inayotazamiwa kuanza Agosti 22 zitalazimika kupambana ili kushiriki kikamilifu ligi hiyo.

Awali kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom ilikuwa mdhamini wa Ligi hiyo kwa miaka mitatu, lakini haijasaini mkataba mpya.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi inayomamia ligi ya Tanzania, Boniface Wambura amesema mazungumzo yanaendelea na kampuni nyingine na uamuzi utatangazwa baada ya kuafikiana.

“Ligi itaanza tukiwa na wadhamini wenza wawili, Azam TV na benki ya KCB, tunaendelea na mazungumzo na wadhamini wengine na tukifanikiwa tutawajuza wadau wa mpira,”amesema Wambura.

Mechi ya ufunguzi wa ligi hiyo itachezwa Agosti 22 katika Uwanja wa Uhuru, Jijini Dar es salaam baina ya mabingwa watetezi Simba na Tanzania Prisons ya Mbeya.