MALAWI-SOKA-MADONNA

Madonna kufungua kituo cha soka Malawi

Mwimbaji na mtunzi wa nyimbo, Madonna
Mwimbaji na mtunzi wa nyimbo, Madonna Irish Times

Mwimbaji, mtunzi wa nyimbo na mwigizaji raia wa Marekani Louise Ciccone maarufu kwa jina la Madonna anatarajiwa kufungua kituo cha soka nchini Malawi.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo imekuja baada ya mwanamama huyo mwenye umri wa miaka 60 kufanya ziara nchini Malawi, tayari Madoona amemuasili kijana wa miaka 12 kutoka Malawi, David Banda.

Madonna amesema ameamua kuchukua uamuzi huo baada ya kupata mawazo kutoka kwa David ambaye kwa sasa anacheza soka la vijana katika akademi moja nchini Ureno.

Shirikisho la soka nchini Malawi limesema limepokea kwa furaha uamuzi wa Madonna ambao unalenga kusaidia kuinua soka la vijana nchini humo.

“Tuna furaha sana kwa hatua hii ambayo itakuwa fursa kwa maendeleo ya soka letu, itaendeleza jitihada za kuinua soka la vijana nchini Malawi,”amesema, Walter Nyamilandu, rais wa Chama cha soka nchini Malawi.