SOKA-TANZANIA
Simba na Mtibwa Sugar kuchuana kesho katika mchezo wa ngao ya hisani
Imechapishwa:
Mabingwa watetezi wa Ligi ya Tanzania Simba SC kesho watashuka kwenye Uwanja wa CCM Kirumba kuchuana na Mtibwa Sugar katika mchezo wa ngao ya hisani, unaoashiria kuanza kwa msimu mpya wa ligi hiyo.
Matangazo ya kibiashara
Simba ni mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania na Mtibwa Sugar ni mabingwa wa Kombe la Shirikisho.
Timu zote mbili tayari zimewasili mkoani Mwanza kwa ajili ya mchezo huo unaotabiriwa kuwa na ushindani mkali.
Simba iliweka kambi nchini Uturuki na Mtibwa Sugar iliweka kambi Mkoani Morogoro kujiandaa na mchezo.