SOKA-YANGASC-CAF

Yanga yapania kupata ushindi dhidi ya USM Algers

Klabu ya Yanga itashuka katika Uwanja wa Taifa kuchuana na USM Algers ya Algeria katika mchezo wa kundi D wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika utakaochezwa Jumapili Agosti 19 saa moja kamili usiku katika Uwanja wa Taifa.

wachezaji wa yanga wakishangilia ubingwa wa Ligi kuu misimu iliyopita
wachezaji wa yanga wakishangilia ubingwa wa Ligi kuu misimu iliyopita yanga
Matangazo ya kibiashara

Mchezo huo utakuwa wa tano kwa Yanga ambayo inashika mkia katika Kundi D ikiwa na alama moja baada ya kushuka uwanjani mara nne.

Kuelekea mchezo huo, Yanga iliweka kambi ya wiki mbili mkoani Morogoro ambapo Ofisa Habari wake Dismas Tena amewaambia wanahabari kuwa Yanga iko tayari kwa mchezo huo.

“Wachezaji wote wako kwenye hali nzuri na tumefanya maaandalizi ya kutosha,”amesema Ten.

USM Algera itakuwa ikiwania kupata alama moja ili kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ya pili kwa ukubwa kwa ngazi ya klabu barani Afrika.